Somalia Hassan Sheikh Mohamoud alilakiwa na waziri wa usalama wa ndani wa Kenya bwana Joseph Nkaisserry
Alipowasili Daadab rais wa Somalia Hassan Sheikh
Mohamoud alilakiwa na waziri wa usalama wa ndani wa Kenya bwana Joseph
Nkaisserry waziri wa maswala ya nje wa Somalia na Balozi wa Somalia
nchini Kenya miongoni mwa viongozi wengine.
Mwandishi wa BBC
Bashkash Jugsoday aliyeko Garissa nchini Kenya anaelezea alivyopokewa
kwa furaha na bashasha huko Garissa siku ya mwanzo wa mfungo wa
Ramadhan. Ziara ya Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamoud inafuatia shinikizo la kenya kutaka kuifunga kambi hiyo
Kambi hiyo ilizinduliwa yapata miaka ishirini na
tano iliyopita ilikuwapa uhifadhi raia wa Somalia ambao walikuwa
wakitoroka mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Hata hivyo, hivi karibuni, serikali ya Kenya imesema wakati umefika kwa kambi hiyo kufungwa. Rais wa somalia alipokewa na viongozi
Kenya inalalamikia utovu wa usalama kufuatia
habari za kijasusi zilizodai kuwa wanamgambo wa Al Shabaab wanatumia
kambi hiyo ya wakimbizi kubwa zaidi nchini Kenya kupanga mashambulizi ya
kigaidi nchini Kenya.
Awali mpango sawa na huu wa kuwarejesha
kwao wakimbizi haukufaulu huku serikali ya Kenya ikilaumu washirika wake
yaani Serikali ya Somalia naShirika la Umoja wa mataifa
linaloshughulikia maswala ya wakimbizi,UNHCR kwa utepetevu. Kambi hiyo ilizinduliwa yapata miaka ishirini na tano iliyopita
Kenya inasisitiza kuwa ina haki ya kimsingi ya
kuwalinda raia wake mbali na kuwa na jukumu la kuwapa hifadhi wakimbizi
ambao sasa wamanza kuhujumu usalama wake.
Aidha Serikali ya Kenya inasema kuwa mazingira yameharibiwa sana katika eneo hilo lenye ukame. Kambi hiyo ilizinduliwa yapata miaka ishirini na tano
Juma lililopita Waziri wa usalama wa ndani wa Kenya
bwana Joseph Nkaisserry alikariri kauli ya serikali yake kuwa hakutakuwa
na mazungumzo zaidi kuhusiana na hilo.
Waziri huyo aliambia BBC
kuwa serikali kwa ushirikiano na serikali ya Somalia na kitengo
kinachoshughulikia maswala ya wakimbizi cha Umoja wa Mataifa UNHCR
zitahakikisha uhamisho huo inafanyika kwa njia nzuri. Kenya inalalamikia utovu wa usalama
Kenya tayari imetenga takriban dola milioni kumi
kufanikisha shughuli hiyo ambayo inasema kuwa inalenga kuihakikishia
usalama wake kufuatia msururu wa mashambulizi ya kigaidi yanayotekelezwa
na wapiganaji wa kundi la al Shabaab.
Chanzo BBC.
BOFYA PICHA HAPA CHINI UONE PICHA ZA UCHI BONGO HASA USWAZI
DON'T FORGET TO LIKE THE PAGE IN ORDER TO GET NEWS UPDATES HAPPEN AROUND THE WORLD
Chapisha Maoni