Rais wa
Marekani,Barack Obama amesema shambulio la risasi katika Klabu ya usiku
mjini Orlando ni la kigaidi na ni kitendo cha chuki
Takriban watu
50 wamepoteza maisha na wengine 53 wamejeruhiwa siku ya Jumapili, baada
ya mtu mmoja aliyekuwa na silaha kufyatulia risasi Klabu moja ya usiku
iliyokuwa ikiwakutanisha watu wa mapenzi ya jinsia moja mjini Orlando
nchini Marekani.Polisi nchini humo wamesema kuwa ni shambulio baya kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo.
Rais Obama amesema Marekani inaungana ikiwa na huzuni,mshtuko mkubwa na inalenga kutetea watu wake, pia amesema mauaji hayo yanawakumbusha ni namna gani ilivyo rahisi kupata silaha hatari nchini Marekani.
Shirika la kijasusi nchini humo,FBI limemtambua mshambuliaji huyo kuwa raia wa Marekani,Omar Mateen ambaye naye aliuawa wakati wa mapambano na vikosi vya usalama katika klabu hiyo ambayo ilikuwa na zaidi ya watu 300 ndani yake.
Chanzo BBC BOFYA PICHA HAPA CHINI UONE PICHA ZA UCHI BONGO HASA USWAZI
Chapisha Maoni